Nahodha wa timu ya Taifa ya Mexico, Rafael Marquez  ni miongoni mwa watu 22  wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao hatari wa wauza madawa ya kulevya duniani.

Marquez mwenye umri wa miaka 38, anahusishwa na tuhuma hizo pamoja na taasisi 43 za nchini Mexico, ikiwemo timu ya mpira wa miguu na Casino.

Uchunguzi ambao umefanywa kwa miaka mingi na kitengo cha upelelezi wa makosa ya dawa za kulevya cha Marekani chini ya Raul Flores Hernandez kimetaja jina la mchezaji huyo kuwa ni miongoni mwa watu wakubwa katika mtandao wa wauza unga duniani.

Marquez  ni mchezaji wazamani wa klabu ya Barcelona, New York Red Bulls ambapo kwa sasa ni beki wa Atlas inayoshiriki ligi ya Mexico  pamoja na nahodha wa timu ya taifa.

Mchezaji huyo amesema kuwa “Sihusiki na lolote katika makundi hayo ya madawa ya kulevya hata hivyo leo ni siku yangu muhimu kwa timu yangu kwa kuwa tunamchezo mgumu mbele yetu na nitatumia nafasi hiyo kudhihirisha kuwa sihusik”, alisema Rafael Marquez.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *