Mchezaji wa Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka mchezaji bora katika mechi ya jana dhidi ya Angola amebainika hatumii dawa ya aina yoyote ya kusisimua misuli baada ya kufanyiwa vipimo.

Mchezaji huyo kwenye mechi ya jana ameshinda goli la pili na kusaidia Serengeti Boys kuibuka na ushindi wa 2-1.

Winga huyo aliwaweka kwenye wasi wasi maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kuonesha kiwango kikubwa cha uchezaji.

Kitendo hicho kilisababisha kupelekwa katika vipimo mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa na kusababisha kushindwa kuenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora ‘Man of the match’ na matokeo yake ikabidi  awakilishwe na mlinzi Dickson Job.

Kwenye mehi hiyo iliyofanyika jana Serengeti Boys ilishinda 2-1 na kufikisha point nne baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare na Mali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *