Mchezaji wa klabu ya Hull City, Ryan Mason amefanyiwa upasuaji baada ya kuumia fuvu la kichwa kwenye mchezo dhidi ya chelsea hapo jana.

Mason ambaye aligongana na Gary Cahill wakati wakiwania mpira katika dakika ya 13 na kutolewa nje huku akisaidiwa na mashine ya kupumulia na kupatiwa huduma ya kwanza kwa muda wa dakika 8 kisha akakimbizwa hospitalini.

Taarifa iliyo tolewa na klabu yake ya Hull City zinasema kuwa Mason yupo katika hali nzuri na anategemewa kusalia hospitalini kwa siku kadhaa pamoja na kuwashukuru watoa huduma ya kwanza pamoja na wauguzi wote waliomsaidia mchezaji wao.

Gary Cahill amemtakia Mason afya njema mapema sawa na wachezaji wengine wengi pamoja na kocha wa Chelsea Antonio Conte.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *