Mshambuliaji wa Bolivia, Marcelo Martins alichukua hatua isiyo ya kawaida na kupigwa picha na wapinzani wao Brazil kabla ya mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Mechi hiyo ya kufuzu kwa kombe la dunia ilimalizika kwa sare ya 0-0 ambapo Brazil alikuwa mgeni wa Bolivia.

Martins, kwa sababu ya uraia wa babake, alichezea Brazil hadi alipotimiza miaka 20, kabla ya kuhamia Bolivia.

Martins, 30, ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu ya Wigan hadi 2012 alialikwa kupigwa picha na wachezaji wa Brazil kabla ya mechi kuanza.

Mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia tayari wamefuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *