Mchezaji tenisi raia wa Jamhuri ya Czech, Petra Kvitova anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na kujeruhiwa na kisu na mtu asiyejuliakana.

Mchezaji huyo ni bingwa mara mbili wa michuano ya Wimbledon mwaka 2011 na 2014.

Kvitova mwenye umri wa miaka 26,alifanyiwa upasuaji wa mishipa katika kiganja cha mkopo anaotumia kuchezea tenesi.

Daktari aliyemfanyia upasuaji nyota huyo wa tenisi amesema itachukua miezi mitatu kuweza kuwa tayari tena kushika fimbo ya kuchezea tenesi.

Kwa upande wake msemaji wa bingwa huyo wa zamani ambaye anashika nafasi ya kumi na moja kwa ubora duniani kwenye mchezo huo amesema kwamba afya ya mchezaji huyo itatengamaa baada ya miezi mitatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *