Mcheza mieleka wa WWE, Jimmy Snuka ‘Superfly’ afariki dunia

0
421

Aliyekuwa mcheza mieleka wa WWE, Jimmy Snuka alimaarufu kama ‘Superfly’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.

Wakili wake amesema mwanamieleka huyo aliaga dunia akiwa katika nyumba ya mkwe wake mjini Florida akiwa pamoja na familia yake.

Mwanamieleka huyo alilazwa hospitali katika nyakati tofauti akisumbuliwa na ugonjwa wa kiakili wa Dementia lakini chanzo cha kifo chake bado hakijabainika

Katika taarifa kwenye mtandao wa shirika la WWE imesema imesikitishwa na kifo kilichompata mwanzilishi wa kitengo cha high flying katika ukumbi wamiereka.

Mtoto wake Tamina Snuka, pia nyota wa mieleka, aliandika kwenye mtandao wa Twitter, ‘Nakupenda babangu’ na kuambatisha picha yake na babake kwenye ujumbe wake huo.

Ni chini ya wiki mbili tangu, mashtaka ya mauaji kutupiliwa mbali dhidi yake kuhusiana na kifo cha mpenzi wake mwaka 1983.

Jaji alitoa uamuzi huo baada ya kubaini Jimmy alikuwa na upungufu wa kiakili na hangeweza kuendelea na kesi hiyo ya mauaji ya mpenzi wake Nancy Argentino.

LEAVE A REPLY