Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Ayeiya Poa Poa amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari nchini humo.

Mchekeshaji huyo maarufu wa kipindi cha Churchil ambaye jina lake kamili ni Emmanuel Makori Nyambane.

Ayeiya Poa Poa kama anavyojulikana na mashabiki wake alihusika katika ajali mbaya ya barabarani karibu na chuo kikuu cha Catholic University CUEA.

Mchekeshaji huyo alikuwa na mkewe, msanii Maina Olwenya na mchekeshaji mwengine Paul Wakimani Ogutu kwenye ajali hiyo.

Ayeiya alikuwa akijulikana kwa ubunifu wake na mzaha ambao uliwawacha mashabiki wengi wakicheka hadi kuumwa na mbavu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *