Mchekeshaji maarufu nchini Marekani, Cathy Griffin amefukuzwa kazi na kituo cha runinga cha CNN kwa kitendo chake cha kushika kinyago kilichofanana na sura ya rais wa Marekani Donald Trump.

Kitendo hicho huenda kikamfanya ashtakiwe kutokana na kile kilichotajwa kama kuvuka mipaka ya uhuru wa habari nchini humo.

Mchekeshaji huyo alionekana akiwa amebeba kinyago cha Rais Trump akiwa amekatwa kichwa, jambo ambalo limezua hasira miongoni mwa watu wengi wakiwemo wapinzani na wafuasi wa Trump nchini Marekani.

Baadhi ya watu maarufu nchini Marekani akiwemo Rais Trump mwenyewe, wamekilaani kitendo hicho na kusema ni dhihaka na udhalilishaji kwa familia za wanajeshi na baadhi ya waandishi wa habari wa Marekani waliochinjwa na Kundi la Kigaidi la ISIS.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Ulinzi wa Rais nchini marekani (Secret Service) imesema uchunguzi umekamilika na wanajiandaa kumfikisha mahakamani Cathy Griffin.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *