Mchekeshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias ‘MC Pilipili’ amelazwa katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza baada ya kupata ajali mkoani Shinyanga.

MC Pilipili amepata ajali hiyo baada ya kujaribu kumkwepa mtu aliyekuwa anaendesha baiskeli na kusababisha ajali hiyo ambapo alikuwa na mwenzake ndani ya gari wakati wakirejea jijini Dar es Salaam.

Katibu mkuu wa Kampuni ya Pilipili Events, Stella Maswenga amesema kuwa wamepokea taarifa za ajali hiyo jana jioni.

Maswenga amesema kuwa MC Pilipili alialikwa mkoani Shinyanga kwa ajili ya kusherehesha harusi mkoani humo na amepata ajali wakati akienda mkoani Mwanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *