Klabu ya Yanga kesho Jumamosi watamuaga beki wao kiraka ambaye ni raia wa Rwanda, Mbuyu Twite baada ya kumaliza mkataba na timu hiyo.

Twite alisajiliwa mwaka 2012 anaondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba wake na ataagwa rasmi kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU kutoka Z anzibar kesho.

Mchezo huo wa kirafiki utapigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na utaanza saa 10 kamili jioni.

Viingilio vya mtanange huo kuwa ni shilingi 5,000/ kwa mzunguko na shilingi 10,000/= kwa VIP huku ukiongeza kuwa tiketi za mchezo huu zitakuwa ni za kielectroniki kwa kadi za Selcom.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *