Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea (CUF) amelitaka Jeshi la Polisi kuruhusu mara moja mchakato wa kwenda kufanya usafi katika Ofisi za CUF zilizopo Buguruni Jijini Dar es salaam.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Simon Sirro kupiga marufuku zoezi hilo na kuwataka wakafanye usafi majumbani mwao na mitaani.

Aidha, wanachama waliotaka kwenda kufanya usafi katika Ofisi hizo wa wale wanaomuunga mkono Maalim Seif Sharif Hamad ambao wanamtaka Prof. Ibrahim Lipumba kuziachia Ofisi hizo.

“Nawapa Polisi wiki mbili, yaani siku 14, ndani ya wiki hizo mbili kuturuhusu kufanya sisi kwenda kufanya usafi na ikiwezekana watusindikize, kama hawataweza basi wazifunge Ofisi hizo zisitumiwe na mtu yeyote,”.

Mbunge huyo amesema kuwa kama wangeenda kufanya usafi na wakakuta watu ambao wasinge wapa ushirikiano basi nao wange wahesabu ni takataka hivyo wangelazimika kuwaondoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *