Mbunge wa Jimbo loa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi amenusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Iyunga jijini Mbeya baada ya gari lake kufeli break na kumgonga mtoto  ’15’ ambaye amefariki wakati akipelekwa hospitali.

Aidha taarifa hiyo inaeleza kuwa askari polisi wanne wamejeruhiwa baada ya kupata ajali wakati wakielekea kwenye ajali hiyo aliyopata mbunge Joseph Mbilinyi  ‘Sugu’

Pia imeelezwa kuwa, Mbunge Sugu ametoka akiwa salama huku dereva wake aliyekuwa akiendesha gari hilo, Gabriel Andrew (43) anashikiliwa na Jeshi la  Polisi mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *