Mbunge wa Dodoma Mjini, Athony Mavunde amekabidhi vitanda vya hospitali na vyandarua vyenye thamani ya shilingi 3,500,000 kwa zahanati na vituo vya Afya 20 katika jimbo la Dodoma Mjini.

Mbunge huyo amesema kuwa amefanya hivyo ili kutatua changamoto ya ukosefu wa vitanda katika jimbo hilo la Dodoma Mjini hali iliyokuwa inasababisha usumbufu wa wagonjwa pindi wanapotakiwa kupumzishwa katika zahati hizo.

Mavunde amesema kuwa vitanda hivyo vitasaidia kuboresha huduma ya Afya haswa maeneo ya pembezoni mwa Manispaa ya Dodoma hivyo kuondoa usumbufu kwa wagonjwa wanapotakiwa kulazwa.

Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde akimkabidhi vitanda mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi.
Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde (katikati) akimkabidhi vitanda mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi amemshukuru mbunge huyo kwa jitiahada zake katika kuwahudumia wananchi wa Dodoma .

Pia Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari Manispaa ya Dodoma imeagiza magodoro kutoka MSD kwa ajili ya vitanda hivyo ili wananchi waanze kuvitumia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *