Mbunge wa Singida Magharibi (CCM) Elibariki Kingu amesema kuwa yupo tayari kufukuzwa ndani ya chama chake cha CCM kwa kupinga uhalali wa elimu ya Mkuu wa Mkoa wa dar es Salaam.

Kingu amesema anasikitishwa na ukimya uliotanda miongo mwa wanachama wa CCM kwa hofu ya kufukuzwa uanachama na kuacha Rais Magufuli akisemwa vibaya kila kona ya nchi kwa sababu ya kiongozi mmoja ambaye elimu uhalali wa elimu yake unatiliwa shaka.

 

Mbunge ameongeza kuwa anakerwa na kusikitishwa na kelele zinazoendelea mitandaoni kuhusu tuhuma za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kughushi vyeti vyake vya taaluma huku matusi na kejeli zikipelekwa kwa Rais, na bado wana CCM wako kimya.

 

Pia ameonesha kukerwa na kile alichokiita matendo yanayokiuka utawala wa sheria yanayofanywa na mkuu huyo wa mkoa.

Kauli hiyo ya mbunge huyo imekuja kufuatia tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu elimu yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *