Mbunge wa jimbo la Babati mjini, Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake kupinduka mkoani Manyara.

Gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo.

Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati.

Kwa upande mwingine huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *