Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu na mke wake Anna Jacob wametoa ushauri kwa wanandoa kufuatia Siku ya Wapendanao'(Valentine’s Day) leo Februari 14 kila mwaka.

Wawili hao wameonesha jinsi wanavyopendana huku wakisimulia jinsi walivyokutana, ambapo wamesema kuwa walikutana kwenye msiba, na kila mmoja akatokea kumpenda mwenzake bila kujali hali zao za kimaisha, takriba miaka 9 iliyopita.

Anna ametoa ujumbe kwa mabinti ambao hawajaolewa kwa kumesema katika mapenzi, haitakiwi mwanamke kumpenda mwanaume kwa sababu ya mali na ndiyo maana yeye alimpenda Kingu wakati huo hajawa mbunge, huku akibainisha kuwa alilazimika kubadili dini, ili wawe pamoja.

Pia Bi. Anna ambaye kitaaluma ni mtaalam wa masuala ya benki (Banker) amesisitiza suala la uaminifu katika ndoa, akiwataka watu wote walio katika ndoa watambue kuwa kilichowaunganisha ni uaminifu, hivyo hawapaswi kuvunja kiapo hicho huku akiweka wazi kuwa kosa pekee ambalo hawezi kulisamehe kwa mume wake ni la kuvunja uaminifu.

Kwa upande wake Kingu, ameshauri wanandoa kuwa na uwazi katika kila jambo ikiwa ni pamoja na mali pamoja na kipato cha kila mmoja, huku akitupia lawama wanaume wengi ambao huwa na tabia ya kuwaficha wake zao baadhi ya mambo kuwa ni hatari na ni sababu ya ndoa nyingi kuvunjika, pamoja na wanaume wengi kufariki kwa shinikizo la daumu na kuacha wanawake wengi wakiwa wajane.

Pia Kingu amewasihi wanandoa kuwa na moyo wa kuvumiliana na kuchukuliana mapungufu ili kulinda ndoa, ambapo ametolea mfano jinsi mke wake alivyombadilisha kutoka kuwa na tabia ya hasira za haraka hadi hakuwa mtulivu, na sasa anajigamba kuwa ni baba bora kutokana na aina ya mke aliyempata.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *