Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hamphrey Polepole ameombwa kufukisha kilio cha wakazi wa Jimbo la Mbulu vijijini kwa Serikali ili wapatiwe chakula cha msaada kukabiliana na njaa.

Ombi hilo limetolewa jana na mbunge wa Jimbo hilo, Fratei Massay wakati katibu huyo alipofanya ziara katika Wilaya ya Mbulu kwa ajili ya kuimarisha Chama Cha Mapinduzi na kusikiliza kero za wananchi.

Mbunge huyo amesema kuwa kwasasa wananchi wanawakati mgumu kutokana na bei ya chakula wanachonunua kutokana na ukame uliokithiri wilayani humo hivyo ameiomba serikali iwapatie chakula cha bei nafuu.

Pia amesema kuwa wananchi wa Jimbo hilo ni hodari wa kulima mazao mbali mbali ya chakula na biashara ila kutokana na ukame ulitokea mwaka jana umesababisha ukosefu wa chakula ndani ya jimbo hilo.

Kwa upande wake Polepole amesema kuwa suala la watu kupatiwa chakula cha njaa bei nafuu analichukua na kuondoka nalo kwani wakati wa ziara yake ameona mahindi mengi yakiwa yamestawi.

Polepole ameongeza kwa kusema kuwa atalipeleka ombi hilo kwa serikali ili lifanyiwe kazi kama masuala mengine.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *