Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesema hawamtambui wala hawamtaki katika umoja huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyejiuzulu wadhifa huo, kisha kuutengua na kurudishwa na msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.

Aidha wamesema hawategemei kugombana ila wataendelea kuimarisha nguvu ya umoja wao.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipokuwa akitoa tamko kwa waandishi kuhusu msuguano wa kisiasa unaoendelea hivi sasa ndani ya CUF.

Mbowe amesema kwa kuwa umoja huo unaiheshimu CUF, wanamtambua Julius Mtatiro kama Mwenyekiti na Maalim Seif Sharif Hamad kama Katibu Mkuu, hivyo wataendelea kufanya kazi nao.

Amesema kutokana na mgogoro huo ndani ya CUF, wanawaelekeza wanachama wao, viongozi wa kuchaguliwa na wawakilishi waendelee kushirikiana katika azma ile ile iliyozalisha Ukawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *