Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema chama chake kipo tayari kusitisha mikutano na maandamano ya Septemba mosi endapo yataanzishwa mazungumzo kutafuta muafaka.

Mwenyekiti huyo amesema chama chake kipo tayari kusitisha mpango huo na kushiriki mazungumzo yeyote yatakayoanzishwa.

Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai mkoani  Kilimanjaro amesema kama kutakuwa na mazungumzo ya kutafuta muafaka watawaeleza wanachama wao kusitisha mikutano ya Septemba mosi na kuendelea na mikutano ya kawaida.

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mwezi uliopita kilitangaza kufanyika operesheni UKUTA nchi nzima kwa lengo la kupinga kwa kile walichodai kuminywa uhuru kwa demokrasia ndani na nje ya Bunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *