Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amevunja uongozi wa Jimbo la Rungwe ili kukinusuru chama kupasuka kutokana na makundi yanayotishia kukigawa chama hiko.

Mbowe amechukua uamuzi huo jana wakati wa kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya na majimbo wilayani humo na baadaye kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi hadi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya chama mwakani.

Uongozi huo wa muda utaongozwa na  Mwenyekiti Sefu Suleiman, Katibu Mwaijumba Mwaijumba na wajumbe 20 ambao watafanya kazi wilaya mzima hadi uchaguzi mpya u

Kabla ya uamuzi huo, Mbowe alisikiliza hoja za kila mjumbe na kugundua kutoelewana miongoni mwa viongozi, kulikotokana na kura za maoni ngazi ya kata na majimbo kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana.takapofanyika. 

Kwa upande wake Katibu wa Chadema Kata ya Ushirika, Baraka Mwampamba, amesema anaunga mkono uamuzi huo wa Mbowe kwani mpasuko huo ulitishia kukivunja chama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *