Mahakama ya wilaya ya Ilala imetoa barua ya wito kuhudhuria mahakamani kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mkewe Lilian Mtei na aliyekuwa meneja wa Billcanas Steven Mligo kwenye kesi iliyofunguliwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) dhidi yao.

Mbowe na Mkewe pamoja  na Steven Mligo wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kushindwa kutumia mashine za kielektroniki (EFD) kutoa risiti kinyume na kifungo cha 86 cha sheria za usimamizi wa kodi ya mwaka 2015.

Mashtaka mengine ni kuipotosha mamlaka ya mapato kutoa nyaraka za uongo kinyume na kifungu 84 na kushindwa kutekeleza masharti ya sheria wa usimamizi wa kodi kinyume na kifungu cha 82 cha sheria hiyo.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutenda makosa hayo Mei 2016 jijini Dar es Salaam ambapo inadaiwa kuwa toka kesi hiyo itajwe mahakamani hapo washiktakiwa hawajawahi kuhdhuria mahakamani hapo.

Wakili wa TRA Marcel Busegano ameilelezea mahakama kuwa wamejaribu kuwapelekea washtakiwa hati ya wito za kufika mahakamani mara nne lakini wameshindwa kufika mahakamani.

Washtakiwa hao wanatakiwa kufika mahakamani hapo Machi 21 mwaka huu kutokana na wito huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *