Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefunguka na kuweka wazi sehemu alipo dereva wa Tundu Lissu, Simon Mohamed Bakari.

Mbowe amesema kuwa kwa sasa dereva huyo yupo nchini Kenya akipatiwa huduma za kisaikolojia kufuatia kushuhudia tukio hilo la kinyama.

Mbowe amesema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari ambapo ameweza kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu sakata hilo na kusema kuwa waliona ni busara kumchukua dereva huyo na kuwa naye nchini Kenya kwa ajili ya kupatiwa msaada huo hadi watakapooona hali yake ya kiafya na uhakika na usalama wake ndiyo anaweza kurejea nchini Tanzania.

Mbali na hilo Mbowe amewataka wabunge wa upinzani kuwa na tahadhari kubwa akidai kuwa kama wasipokuwa makini huenda kiongozi mwingine anaweza kupata matatizo kama hayo hata hivyo amesema kuwa tamko la chama chake litakuja karibuni.

Freeman Mbowe.
Freman Mbowe amedai kuwa Tanzania si sehemu salama tangu umefanyika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 na kudai kuanzia hapo yalianza kujitokeza kwa mauaji ya viongozi kikiwepo kifo cha Alphonce Mawazo Mkoani Geita, Kupotea kwa kina Ben Saanane.

Kutekwa  wasanii na kufanyiwa mateso makubwa pamoja na Wabunge kufungwa na kushtakiwa kila siku.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *