Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amefunguka na kusema kuwa mkoa wa Kilimanjaro hawategemei CCM kwa ajili ya maendeleo ya mkoa huo na kusema kitu pekee ambacho kinafanya mkoa huo kuwa wa mfano kwa mageuzi ni kutokana na elimu.

Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai amesema hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Machame Uroki katika ziara yake ya jimbo na kusema kuwa Kilimanjaro inakuwa kimaendeleo kutokana na baadhi ya wazee miaka hiyo kupata elimu ya kutosha ambayo ndiyo imekuwa chachu ya maendeleo hayo.

“Sifa kubwa ya kwanza katika taifa hili kuhusu mkoa wa Kilimanjaro ni elimu, wazee wetu walisoma siyo wote ila wachache walisoma sana kulinganisha na mikoa mingine kwa hiyo maendeleo ya Kilimanjaro hayategemei CCM.

Ameendelea kusema kuwa maendeleo ya Kilimanjaro yalikuwepo hata kabla ya uhuru watu walisoma siku nyingi na watu walipata imani siku nyingi, sifa hii ni lazima tuirejeshe, tuna shule nyingi lakini shule nyingi ni zile ambazo hazina sifa ya kuitwa shule”.

Aidha Mbowe aliwataka watu kuwekeza nguvu kubwa kwenye elimu kwa watoto wao kutokana na ukweli kwamba ardhi ya kuweza kuwarishisha watoto kwa sasa haipo Kilimanjaro hivyo wanapaswa kuwekeza zaidi na zaidi kwenye elimu na kusema anatambua kuwa wanafanya hivyo ila bado haitoshi wanapaswa kuongeza nguvu zaidi na zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *