Mwanamuziki wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo, Mboyo Moseka maarufu kwa jina la Mbilia Bel ameadhimisha miaka 40 toka aanze kuingia kwenye kazi ya muziki wa Bolingo nchini humo.

Mbilia Bel mwenye umri wa miaka 57 alianza kujiingiza kwenye kazi ya muziki akiwa na umri wa mika 17 akiwa msichana mdogo ambapo hadi sasa ametimiza miaka 40 toka ajiingize kwenye tasnia ya uimbaji.

Mwanamuziki amesema kuwa anatarajia kuachai album yake mpya ya mwisho wiki ijayo inayoitwa ‘Signature’ na badala yake anaachana na kazi hiyo ya uimbaji kwani imeshamfanyia mambo mengi kutokana na uwepo wake kwenye kazi hiyo.

Mbilia Bel amesema kwamba ataendelea kuwa mshauri wa wasichana chipukizi wanawania kuingia katika tasnia ya muziki hivi sasa.

Mwanamuziki Mbilia Bel, alipata sifa kubwa katika miaka ya 70 na thamanini kutokana na sauti yake kukonga nyoyo za watu.

Mbilia Bel aliwahi kufanya kazi kwenye bendi ya TabuLey Rochereau chini ya nguli wa muziki huo marehemu Tabu Ley ambaye pia alikuwa mpenzi wake na walibahatika kupata watoto wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *