Mkazi wa Kijiji cha Kiterere tarafa ya Inano wilayani Tarime mkoani Mara, Joel Robert anashikiliwa na Polisi akituhumiwa kuwatapeli watu mbalimbali na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kwa kujifanya wakili wa kujitegemea akionekana kufuatilia kesi za watu katika maeneo ya mahakama na vituo vya Polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ngainz alisema wanamshikilia na kumhoji Robert anayetuhumiwa kuwatapeli watu mbalimbali ambao baadhi yao wamepeleka malalamiko yao Polisi, wakimtuhumu kujifanya wakili wa kujitegemea.

 “Tunawaomba raia wema kuwafichua matapeli hao ambao wanawaibia fedha zao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria na tunawahimiza wananchi mara wanapohitaji kupata msaada wa kisheria waende katika ofisi za mawakili wanaotambuliwa kisheria na wenye leseni ama taasisi zinazoshughulikia mambo ya sheria badala ya kwenda kuwaona matapeli bila kuwatatulia matatizo yanayowakabili,” alisema.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya mahojiano kukamilika.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *