Mshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe amesema kuwa alikutana na kocha Arsene Wenger na kumshawishi ajiunge na Arsenal.

Wakati wa dirisha la usajili Mbappe alihusishwa na kwenda katika vilabu vingi kama vile Real Madrid, Manchester City na Arsenal pia walikuwa kwenye mbio za kumnasa Mfaransa huyo lakini alitua PSG.

Mbappe aliongeza kuwa alitaka kujiunga na Arsenal ili kukuza kiwango chake lakini baada ya kuongea na familia yake na kushauliwa afanye chaguo sahihi kwake aliona PSG ndio chaguo sahihi.

Wenger alikuwa akimfatilia kwa karibu kinda huyo mwenye umri wa maika 18 ili kutaka kumsajili na ililipotiwa kuwa kocha huyo alikutana na Mbappe na walifanya mazungumzo kwa takribani masaa matatu katika mji mkuu wa Ufaransa.

Hata hivyo iko wazi kwamba ni ngumu kwa Arsenal kutoa kiasi cha pesa kama PSG na mshambuliaji huyo amejiunga na PSG kwa mkopo kabla ya kukamilisha usajili wa kudumu kwa pauni milioni 165 msimu ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *