Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Mb Dogg amewataka mashabiki wake wamvumilie kwa kipindi hiki ambacho yupo kimya kwa muda mrefu.

Mb Dog amesema kuwa muziki ni kama upepo na kipindi hiki upepo huo wa muziki haupo upande wake hivyo mashabiki zake wamuelewe.

Pia amesema muziki ni kama maisha kuna kipindi cha kupanda na kushukma na kwamba kipindi hiki upepo haupo wakati wake hivyo mashabiki zake wanapaswa kumuelewa na kutambua kwamba kwa sasa upepo upo upande wa pili.

Ameongeza kwa kusema kuwa kuwa kuna mipango ambayo anaipanga kwa sasa na menejimenti yake na mambo yakikaa sawa atarudi kwenyeanga ya muziki wa Bongo kwa kuwa sasa kuna simu nyingi zinamuhamasisha kurudi kwenye muziki.

Mb Dog ni miongoni mwa wanamuziki waliofanya vizuri kipindi cha nyuma akiwa katika kundi la Tip Top Connection ambapo alitamba na nyimbo kama Ratifa, Waja na nyingine kibao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *