Mke wa mwanamuziki wa hipo hop nchini Marekani, T.I ambaye alikuwa muimbaji wa kundi la Xscape aitwae Tiny amedai talaka kutoka kwa mumewe huyo baada ya kutoolewana kwa wawili hao ndani ya ndoa yao.

Taarifa za kuingia dosari kwa ndoa hiyo baada ya kuonekana picha zikimuonesha Tiny akicheza na Floyd Mayweather ambaye hana mahusiano mazuri na T.I kwenye party ya Mariah Carey siku za karibuni.

Wawili hao wamefanikiwa kupata watoto watatu ambao wawili ni wanaume na mmoja mwanamke baada ya kufunga ndoa mwaka 2010 nchini Marekani.

Licha ya kuachana kwa mastaa hao bado watakuwa na mawasilino kuhusu kuwalea watoto hao kutokana na sheria za nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *