Bondia Floyd Mayweather amenunua nyumba mpya ya kifahari yenye thamani ya paundi milioni 18.9 (zaidi ya Sh bilioni 56) katika eneo la Beverly Hills.

Jumba hili jipya alilonunua, lina vyumba sita vya kulala na mabafu kumi. Pia lina chumba maalumu cha sinema ambacho wanaweza kukaa watu 50 kwa raha kabisa.

Mayweather amecheza ngumi kwa miaka 21 na alistaafu Agosti 26 akiwa ameingiza fedha nyingi zaidi ya bondia yeyote yule kihistoria

Muonekano wa ndani wa nyumba hiyo aliyonunua Mayweather.
Muonekano wa ndani wa nyumba hiyo aliyonunua Mayweather.

Mmarekani huyo anadai kuwa yeye ndiye bondia wa kwanza kuingiza zaidi ya dola bilioni moja (zaidi ya Sh trilioni 2) katika mchezo huo mgumu zaidi.

Ukiachana na mkwanja aliotumia katika kununua jumba hilo, inasemekana pia kuwa May­weather ametumia kiasi cha pauni 369,000 (zaidi ya Sh bilioni moja) kwa ajili ya kununua vitu vya ndani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *