Bondia Floyd Mayweather amefunguka kuhusu maisha yake ya ndondi na binafsi ikiwemo kuhusu kama atarejea kwenye ndondi au ndiyo amestaafu ukweli.

Mayweather ambaye alitangaza kustaafu kupigana mwaka 2016 kisha kuamua kurejea mwaka huu na kupigana pambano dhidi ya Conor McGregor likiwa ni pambano lake 50, inaaminika ndiye bondia mwenye mafanikio makubwa kifedha kuliko wote kuwahi kutokea.

Katika pambano hilo lililopewa jina la pambano la fedha, Mayweather alishinda na hivyo kujiandikia rekodi ya kucheza mapambano 50 akishinda yote, huku akiingiza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na mikataba mbalimbali.

Mayweather amedai kuwa hadi sasa ana wapenzi saba na ana magari 25 ya kifahari ambayo yote yapo Las Vegas.

Magari hayo ni yale ambayo anayo kwenye jiji hilo tu, yakiwemo Bugatti na Ferrari ambayo thamani yake ni zaidi ya shilingi bilioni 1 kila moja.

Mayweather amesisitiza kuwa, pambano lake na McGregor lililofanyika mwezi uliopita ndilo lilikuwa la mwisho kwake na hana mpango wa kurejea ulingoni kupigana.

Mayweather amesema hayo katika ukumbi wa usiku wa Mayweather unaojulikana kwa jina la Girl Collection unaopatikana Las Vegas.

Alipoulizwa kuhusu mpenzi wake, alisema yeye ni mwanaume ambaye hawezi kuwa mwaminifu kwa mwanamke mmoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *