Kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga amesema timu yake iko tayari kupambana dhidi ya Rwanda, leo Jumamosi na kuibuka na ushindi katika mchezo huo.

Taifa Stars inacheza mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan), dhidi ya Rwanda kwenye Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini hapa.

Mayanga amesema kuwa kutokana na timu yake kufanya mazoezi kwa siku nne mfululizo, imani yake kuwa ni kufanya vizuri dhidi ya Rwanda.

Katika hatua nyingine, Mayanga amewasifia wachezaji aliowaongeza katika timu yake baada ya kumalizika kwa Michuano ya Cosafa kwa kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani.

Mayanga amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuishangilia Taifa Stars ikicheza dhidi ya Rwanda maarufu kama Amavubi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *