Mawaziri watatu nchini Gambia wajiuzuru

0
229

Mawaziri watatu nchini Gambia wamajiuzulu wakati Rais Yahya Jammeh akipuuza wito wa kumtaka aondoke madarakani wakati muhula wake utakapokamilika siku ya Alhamisi.

Mawaziri hao waliojiuzuru ni waziri wa masuala ya nchi za nje, waziri wa fedha na waziri wa biashara ambao wote wamejiuzulu leo.

Wiki iliyopita waziri wa habari Sheriff Bojang na Alieu Jammeh wa michezo nao walijiuzulu.

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia kwenda nchi jirani ya Senegal na hadi nchini Guinea-Bissau, kutokana na hofu kuwa huenda kukazuka ghasia.

Mfanyabiashara Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal ameapa kuchukua madaraka.

Barrow alimshinda Yahya Jammeh ambaye aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi mwaka 1994.

LEAVE A REPLY