Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, hivi karibuni alionekana kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo dhidi ya JKT Ruvu uliofanyika Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Mavugo alivunja kanuni ya shirikisho hilo baada ya kuvaa jezi namba 11.

Hii ilikuwa namba tofauti na ile ambayo aliivaa kwenye mchezo dhidi ya Ndanda ambapo alivaa namba 9 ambayo ilisajiliwa kihalali kuwa ni namba yake.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB), Boniface Wambura amesema kitendo hicho cha Mavugo kuvaa jezi zenye namba mbili tofauti katika mechi mbili tofauti za ligi hiyo ni kosa kubwa, hivyo wanamchunguza na anaweza kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mavugo amesema hakujua kama ni kosa lakini anachoweza kusema ni kwamba aliamua kuitumia jezi namba 11 na kuachana na namba 9 kwa sababu ilikuwa akiipenda tangu zamani.

Kwa mujibu wa kanuni ya 60 ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2016/17, inayozungumzia usajili wa wachezaji kupitia vifungu vya 11 na 12 vinalitolea ufafanuzi suala hilo.

Kifungu cha (11) cha kanuni hiyo ya 60 kinasema kuwa: “Kila mchezaji wa ligi kuu atatakiwa kuwa na namba moja ya kudumu ya jezi ya kuchezea iliyosajiliwa na klabu yake wakati wa maombi ya usajili wa wachezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *