Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo amewasili jana usiku nchini kwa ajili ya kujiunga na Simba SC baada ya tetesi za muda muda mrefu.

Mchezaji huyo amewasili Saa 4:30 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kupokewa na Makamu wa Rais wa Simba, Geoffrey Nyange “Kaburu”.

Leo Mavugo anatarajia kufanya mazungumzo na uongozi wa Simba SC kabla ya kwenda kambini mkoani Morogoro kujiiunga na timu hiyo.

Baada ya mpango wa kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili nchni Ufaransa maarufu kama Ligue 2 kukwama mchezaji huyo ameamua kujiunga na Simba SC.

Mchezaji huyo alikwenda Ufaransa wakati tayari Simba SC wamesema wamekwishaingia Mkataba nae kuanza kuwatumikia kuanzia msimu ujao.

Simba SC ipo kambini mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *