Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Laudit Mavugo amesema kwamba sasa yupo katika timu nzuri zaidi maishani mwake baada ya kusaini ndani ya klabu hiyo.

Baada ya kuisaidia Simba SC kushinda 4-0 dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kwenye mchezo wa kirafiki, Mavugo amesema kwamba amefurahia mwanzo mzuri katika timu ya Msimbazi.

Mavugo amesema kwamba amefurahi na amekuwa na mwanzo mzuri katika timu kwani ametokea benchi na amekwenda kufunga na zaidi timu imecheza vizuri sana, na anaweza kusema hii ni timu nzuri zaidi.

Mshambuliaji huyo aliyetokea Vital’O ya ya Burundi amesema kwamba sasa anaelekeza nguvu zake katika kuisaidia Simba SC kushinda mataji ambayo timu hiyo inashiriki kwa kushirikiana na wachezaji wenzake.

Simba SC jana ilisherehekea miaka 80 toka kuanzishwa kwa timu hiyo na kuifunga AFC Leopard ya Kenya mabao 4-0 katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *