Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewalaumu washambuliaji wake baada ya kukosa magoli kwenye mechi dhidi ya Anderlecht ambapo walitoka 1-1 kwenye mechi hiyo ya kombela Europa ligi.

Manchester United walikuwa wakwanza kupata bao na Anderlecht wakasawazisha katika dakika za mwisho za mechi ya robo fainali.

United iliongoza 1-0 nchini Ubelgiji hadi dakika 86 wakati waandalizi wa mechi hiyo waliposawazisha ikiwa ni shambulio lao la kwanza.

Maurinho amesema kuwa iwapo angekuwa mlinzi wa man united angekasirishwa sana na washambuliaji.

Kocha aliongeza kwa kusema kuwa mabeki walifanya kazi ya kutosha lakini washambuliaji wakashindwa kuamua matokeo ya mechi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *