Ni kama Bongo Fleva INAZALIWA UPYA vile. Ukitazama kwa sasa, Bongo Fleva imeanza kubadilisha muelekeo na WAKONGWE wanaonekana kuanza kuchukua nafasi zao.

Baada ya Lady Jay Dee kuwa mmoja wa mastaa waliotisha kwa ngoma NDI NDI NDI mwaka 2016 na Ali Kiba akikusanya tuzo kibao kwa ngoma moja tu, AJE ni dhahiri wakongwe nafasi zao zilichukuliwa walipoenda likizo.

Lakini Matonya anataka kwenda HATUA MOJA mbele zaidi, anaitaka REMIX ya Anitha kwani Anitha wake a.k.a Lady Jay Dee ‘amekuwa mcharo’.

Staa huyo wa zamani wa Tip Top Connection amedai kuwa ‘anamtafuta kwa udi na uvumba’ Lady Jay Dee ili wayapangane na wairudishe HIT ya ANITHA kwenye soko.

Je, endapo Jay Dee atakataa, Matonya atafanyaje? Waswahili husema ‘mtumai cha ndugu, hufa maskini’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *