Matonya amaliza tofauti zake na Adam Juma wa Visual Lab

0
538

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva, Matonya amesema kuwa amemaliza tofauti zake zilizokuwa kati yake na director maarufu nchini Adam Juma baada ya kudumu kwa muda mrefu.

Matonya amesema kuwa kwa sasa hana ugomvi kati yake na Adam Juma kwa sababu umemalizika na kwamba akipata nafasi atafanya naye kazi tena kama kawaida kwani hana shida kabisa.

Adm Juma: Muongozaji wa video za Bongo fleva kutoka kampuni ya Visual Lab.
Adam Juma: Muongozaji wa video za Bongo fleva kutoka kampuni ya Visual Lab.

Mwanamuziki huyo kutokea pande za Tanga amesema kuwa walisumbuana sana na Adam Juma hali iliyopelekea kufikishana hadi polisi lakini kwa sasa wameshakuwa kama familia

Mkali huyo ameongeza kwa kusema kuwa Adam amefanya mabadiliko makubwa katika sanaa ya bongo fleva na sasa ameamua kufanya na waadaaji wengine ili aweze kubadilika.

Wawili hao walikuwa na tofauti iliyodumu kwa muda mrefu mpaka kupelekana polisi baada ya kugombana kutokana na maslai ya kimuziki.

LEAVE A REPLY