Mechi za kombe la Mfalume jana zimefanyika katika viwanja tofauti nchni Hispania kwa kuzikutanisha timu mbali mbali.

Barcelona waliibuka na ushindi wa kishind wa mabao 7-0 dhidi ya Hercules katika uwanja wa Camp Nou.

Sevilla wakaibuka na ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya timu ya SD Formentera huku mshambulia Luciano Dario Vietto pamoja na Wissam Ben Yedder wote walifunga hatrick katika mchezo huo.

Eibar wao waliibuka na ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Sporting Gijon na Deportivo La Coruna wakashinda kwa ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi Real Betis.

Osasuna wakaibuka wababe kwa kuichapa Granada kwa 2 – 0 Valencia wakashinda kwa mabao 2 – 1 dhidi ya Leganes.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *