Kiungo mpya wa Manchester United, Nemanja Matic amesema kuwa anataka kucheza ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu.

Matic ambaye alikuwa mchezaji bora wa mechi dhidi ya West Ham wiki iliyopita ambapo United ilishinda 4-0 amesema kuwa anawashukuru wachezaji wenzake kwa kumpa ushikiano toka awasili kwenye klabu hiyo.

Kiungo huyo amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano wanaompa toka siku ya kwanza ajiunge na mashetani hao huku akisema kuwa wamemsaidia sana mambo mengi.

Ikiwa ni mara ya kwanza mchezaji huyo kucheza Old Trafford amesema kuwa amejisikia furaha sana kucheza katika uwanja huo huku amevaa jezi ya timu hiyo kwasababu ni timu kubwa na bora duniani.

Akimzungumzia mchezaji mwenzake Lukaku, Matic amesema kuwa anafurahishwa na mshambuliaji huyo kutokana na ubora wake aliouonesha ndani ya klabu hiyo toka ajiunge msimu uliopita akitokea Everton.

Amesema kuwa Lukaku ni mchezaji mzuri kwani anajua nini anafanya akiwa uwanjani na muda wote anatamani kushinda tu.

Nemanja Matic amejiunga na Manchester United msimu huu akitokea klabu ya Chelsea ambaye ameisaidia timu hiyo kushinda taji la ligi kuu msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *