Mwanamuziki wa Bongo fleva, Mataaluma amesema kuwa anatarajia kurudi kwenye game baada ya kupotea kwa muda mrefu kutokana na kujihusisha na masuala ya biashara.

Mwanamuziki huyo alitamba sana kwa miondoko ya mchiriku kwa ngoma yake ya Kariakoo pamoja na Mama Mbaya amedhamiria kurudi kwenye game la muziki kama ilivyokuwa zamani.

Mataluma amesema alipokuwa kimya kwenye game alikuwa anafanya biashara ya mkaa lakini kutokana na mfumo mpya kuwa mgumu ameamua kurudi kwenye game kwani muziki anaona unalipa kwa sasa kuliko biashara ya mkaa akliyokuwa akifanya.

 

Mataluma aliendelea kuweka wazi kuwa kutokana muziki wa singeli kwa sasa kufanya poa zaidi na yeye alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki huo, hatarudi kwenye singeli bali atafanya mchiriku, ili kuweka utofauti kwenye game.

 

Mataluma amesema “Waanzilishi wa singeli, waanzilishi wa mchiriku mimi ndo wa kwanza kufanya nao kwa sababu hii bongo fleva unayoisikia mi ndo mtu wa kwanza kuimba na Manfongo na Msaga Sumu, mi ndo wa kwanza kwa hiyo wasione ajabu na mimi niko vizuri.

 

Pia ameongeza kwa kusema sijaamua kuzitoa hizo kazi ingawa naweza, lakini si kwenye muziki wangu wa mara ya kwanza Mama mubaya na Kariakoo, mi niwaachie kisingeli mi nifanye mchiriku”,.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *