Kiungo wa Manchester United, Juan Mata umekataa mshahara wa pauni 375,000 kwa wiki kujiunga na ligi kuu ya China.

Mata anaonekana kuridhika na maisha ya Mancheter na huenda akaongeza mkataba kuendelea kukipiga na kikosi cha Mourinho.

Amesema kuwa ”Nina furaha hapa kuwa hapa, nimekuwa hapa kwa karibia miaka minne sasa baba yangu amefungua mgahawa wa kihispania na kwakuwa mabo ni mazuri ninafurahia kubaki hapa,”.

Kiungo huyo mshambuliaji alijiunga na Manchester United mwaka 2014 kwa kitita cha Pauni milioni 37.1 akitokea Chelsea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *