Mtayarishaji mokongwe wa muziki nchini, Johackim Kimario ‘Master J’ amefunguka kwa kusema kuwa inamuuma sana kuona washindi wa Bongo Star Search wakishindwa kufanya vizuri kwenye fani hiyo ya muziki.

Master J amedai kuwa sababu kubwa ya washindi hao kushindwa kufanya vizuri ni vipaumbele vyao wanavyoviwekwa baada ya kushinda tofauti na matarajio ya waandaaji wa shindano hilo.

Pia Master J ameongeza kuwa washindi wengi walipopata fedha zao, walikuwa hawaendi kuwekeza kwenye muziki bali kuzitumia fedha hizo kutatua changamoto zao za kimaisha na ndiyo maana wanafeli.

Master J amesisitiza kuwa alimshauri Madam Rita kuwa siku za usoni ni vyema washindi wakapewa fedha nusu na zingine zikatumika kama mtaji wa muziki wao lakini tofauti na sasa ambapo wanapewa pesa zote.

Toka kuanzishwa kwa shindano hilo hakuna hata mshindi mmoja aliyewahi kufanya vizuri kwenye medani ya muziki baada ya kushinda.

Shindano la BSS uandaliwa na kampuni ya Benchmark iliyochini ya Madam Rita ambaye ndiye chief jaji kwenye shindano hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *