Wanamuziki wa Bongo fleva, Tunda Man, Country Boy, na TID wanatarajiwa kukutana kwa pamoja kwenye tamasha ndani ya ukumbi wa maisha Basement uliupo Kijitonyama Dar es Salaam.

Wasanii wengine ni Mesen Selekta, Pam D, Sold ground family, Bob Junior na Haitham pamoja na mastaa wa filamu wakiongozwa na Kajala Masanja.

Mratibu wa shoo hiyo, Geofrey Jilla ‘Jilla the Boss’ alisema kuwa, mbali na uwepo wa wakali hao, mashabiki wa burudani wategemee kupiga picha ‘red carpet’ na mastaa mbalimbali.

Mratibu huyo amesema shoo hiyo pia itawapa fursa wale wote waliozaliwa mwezi wa 11 kukata keki ya pamoja na mastaa hao.

Pia amesema kuakuwa na mamodo wote Bongo wakiongozwa na Kidoa, Lulu Diva, Amber Lulu, Erycah na wengine kibao kwa kiingilio cha 10,000 tu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *