Kocha wa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC Massimiliano Allegri, ameendelea kusumbuliwa na tetesi za kuihama klabu hiyo, na kutimkia kaskazini mwa jijini London mwishoni mwa msimu huu.

Allegri anatajwa kuwa katika mpango wa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger ambaye huenda akaondoka mwishoni mwa msimu huu, pindi mkataba wake utakapomalizika.

Meneja huyo amekua akisumbuliwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi hizo, na mara kadhaa amezijibu kwa kukanusha uvumi huo, ambao ulianza baada ya kuonekana jijini London mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *