Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limethibisha kumshikilia video queen maarufu, Agnes Gerald ‘Masogange’ kutokana na kujihusisha na madawa ya kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa Masogange anashikiliwa na jeshi hilo kutokana na kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Sirro amesema kuwa Masogange alikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Central na leo amepelekwa kupimwa kwa mkemia mkuu na kama akibainika kutumia dawa hizo kesho atafikishwa mahakamani.

Kamanda Sirro amesema kuwa Masogange ni miongoni mwa watuhumiwa 349 waliokamatwa wakijihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya ambapo hadi sasa hivi jumla ya watuhumiwa 16 wamefikshwa mahakamani.

Taarifa za kukamatwa kwa video queen zilienea lakini hakukuwa na taarifa sahihi ya kukamatwa kwa mrembo huyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *