Video model, Agnes Gerald (Masogange) leo anatarajiwa kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi yake ya tuhuma za kutumia dawa za kulevya inapokuja kwa kutajwa na kuangalia kama upelelezi umekamilika au la.

Masogange anatarajiwa kufikishwa mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri wa mahakama hiyo, ambaye ndiye anasikiliza kesi hiyo.

Mara ya mwisho kesi hiyo ilipotajwa mahakamani hapo hakimu huyo alimpa onyo mshtakiwa huyo baada ya kuchelewa kufika katika chumba cha mahakama, hatua iliyofikiwa baada ya Wakili wa Masogange, Nictogen Itege kuieleza mahakama kuwa mteja wake yuko njiani anakuja.

Taarifa hiyo ilisababisha, Hakimu Mashauri kumuhoji kuwa mbona yeye yupo mahakamani? Akadai kuwa walipita njia tofauti ndiyo sababu ikatokea kuwa mmoja kafika mwingine bado.

Hakimu Mashauri alisema mteja wake anatakiwa afuate masharti ya dhamana na mamlaka.

Hata hivyo, baada ya muda kidogo Masogange alionekana katika viwanja vya Mahakama wakati kesi yake tayari ilikuwa imeahirishwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *