Video queen Bongo, Agnes Masogange amesema kuwa ameamua kuachana rasmi na kuuza sura kwenye video kutokana na mpenzi wake kutopenda kazi hiyo.

Masogange amesema kuwa mpenzi wake hapendi kazi hiyo pia amewataka watu kuacha kufikiria kwamba anafanya biashara kujiuza.

Masogange ambaye alipata umaarufu baada ya kuuza sura kwenye video ya Belle 9 amesema kuwa hana dhiki ya kufikia kuuza mwili wake ili apate pesa.

Pia Masogange amesema kuwa alikuwa na biashara zake anafanya na wanaosema anajiuza  hawanisaidii chochote mana hakuna yoyote anayemnunulia kitu chochote.

Masogange ameongeza kwa kusema kuwa “Unajua sisi wadada tuna tabia ya kuoneana wivu akiona unafanya vizuri anaanza kukusemea vitu vya ajabu pembeni.

Katika hatua nyingine mrembo huyo alikana kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Mrembo huyo kwasasa anakabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *