Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ leo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kutumia aina mbili za dawa za kulevya.

Masogange amesomewa mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya ikiwamo heroin mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi, Wilbroad Mashauri.

Video Queen huyo ametimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni 10.

Masogange amefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza baada ya jalada lake kukwama kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa sababu mbalimbali za kisheria.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 22, mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo Kisutu jijini Dar es Salaam.

Masogange alikamatwa na jeshi la Polisi na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi (Central) jijini Dar es Salaam ambapo alipelekwa kwa mkemia mkuu na kupimwa na kugundulika kuwa anatumia dawa za kulevya aina ya heroine.

Video Queen huyo ameingia kwenye orodha ya wasanii walikamatwa kwa kujihisisha na madawa ya kulevya kwenye operesheni iliyoanzishwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *