Kesi ya matumuzi ya madaya ya kulevya inayomkabili video queen wa Bongo, Agness Gerald maarufu kama Masogange imeendelea tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Masogange alipandishwa kizimbani leo kuanza kujitetea lakini wakili wa Serikali, Aldof Mkini aliomba kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine.

Mshtakiwa huyo ataanza kujitetea baada ya mahakama kumkuta na kesi ya kujibu kwa upande wa mashtaka kuleta mashaidi watatu.

Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika maeneo yasiyojulikana katika jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kesi hiyo imepigwa kalenda hadi Novemba 14 mwaka huu ambapo shahidi upande wa utetezi atatoa ushahidi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *